Ujiji
Kutoka Wikipedia
Ujiji ni mji upande wa Magharibi wa Tanzania mwambaoni kwa Ziwa Tanganyika. Ni mahali pa kihistoria na mji wa kale katika magharibi ya Tanzania. Iko kilometa 10 tu upande wa Kusini wa mji wa Kigoma.
[hariri] Historia
Ujiji huaminiwa imeundwa mwanzoni mwa karne ya 19 labda kidogo baada ya mwaka 1821 [(makala "Udjidji" katika DKL]. Ilikuwa mwisho wa njia ya misafara kati ya pwani la Bahari Hindi na Ziwa Tanganyika. Bidhaa kutoka pwani zilihifadhiwa hapa katika ghala na kusambazwa kwa biashara ya kuvukia ziwa kwa mashua. [[ Wapelelezi]] Wazungu walianza kufika wakati wa Tippu Tip. Ni mahali ambapo Richard Burton na John Hanning Speke walifikia Ziwa Tanganyika mwaka wa 1858, na tena ambapo Henry Morton Stanley alimkuta David Livingstone mwaka wa 1871.
Wakati wa ukoloni wa Kijerumani umuhimu wa Ujiji ulipungua. Mwambao ulifaa mashua ya kienyeji lakini kina hakikutosha kwa ajili ya meli mpya. Hivyo makao makuu ya utawala yalipelekwa Kigoma penye bandari nzuri.
Makala hiyo kuhusu "Ujiji" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Ujiji kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |