Karne ya 19
Kutoka Wikipedia
Karne ya 19 ilikuwa kipindi cha miaka mia moja kati ya 1800 na 1900. Kikamilifu kilianza tar. 1 Januari 1801 na kuishia 31 Desemba 1900.
Kama kila "karne" ni kipindi kinachohesabiwa kwa hiari ya kibinadamu kwa sababu ni mgawanyo wa kalenda tu - hali halisi maendeleo na mabadiiliko makubwa hayafuati migawanya ya kalenda ya kibinadamu.
Hata hivyo kipindi hiki cha karne ya 19 kilikuwa kipindi muhimu sana katika historia ya binadamu.
Mabadiliko mengi yalianza Ulaya na kupanua duniani hivyo karne hii imeitwa na wataalamu "karne ya Ulaya".
Kati ya tabia za pekee za karne hii ni kama zifuatazo:
- Mapinduzi ya viwandani yaliwahi kuota mizizi katika Uingereza kabla ya mw. 1800 lakini katika karne hii ilienea katika nchi za Ulaya na kubadilisha uwezo wao
- Nchi zilizopita katika mapinduzi ya viwandani yaliongezeka nguvu za kiuchumi na kijeshi kushinda mataifa nje ya mapinduzi haya
- Mtindo wa ubepari ulipata umuhimu na kugusa maisha ya watu wengi
- Tabaka mpya ya wanafanyakazi ilijitokeza
- Tabaka ya makabaila ilipungukiwa umuhimu wake katika jamii za nchi zilizoshiriki katika mapinduzi ya viwandani
- Maisha ya viwandani na maisha ya mjini yalivunja maisha ya mashambani hivyo mapokeo na desturi nyingi zilizowahi kuendelea tangu karne nyingi
- matunda ya fikra za mwangaza yalisababisha
- kutokea kwa sayansi ya kisasa
- ukosoaji wa dini
- Idadi ya watu duniani ilianza kukua haraka kushinda miaka yote ya historia ya awali kwa sababu ya
- matokeo ya teknolojia na sayansi yaliongeza kiasi cha chakula kilichopatikana kwa watu
- sayansi ya tiba iligundua njia za kupambana na magonjwa na maradhi
- Nchi kadhaa za Ulaya zilitumia nguvu mpya ya kueneza utawala wao wa kisiasa nje ya Ulaya
- Ukoloni ulienea : mwanzoni wa karne hii polepole, mwishoni kwa mbio
- Fundisho jipya ya "utaifa" lilianza kubomoa misingi ya madola makubwa ya kimataifa katika Ulaya kama Uturuki, Austria, Urusi.
- Katika siasa madola kadhaa yaliyowahi kuratibu maisha ya watu tangu karne nyingi yalipungukiwa, kuvunjwa au kupotea kabisa kama vile
- Dola takatifu la Roma la Wajerumani katika Ulaya ya Kati
- Dola la Moghul katika Bara Hindi
- Dola la Uturuki (Uturuki, Afrika ya Kaskazini, Asia ya Magharibi)
- Dola la Hispania (Hispania, Amerika ya Kusini na Ufilipino)
- Dola la Uingereza lilitokea kuwa dola kubwa duniani
- Utumwa ulipungua sana duniani
- Ukristo ulienea upya nje ya maeneo ya Ulaya baada ya kurudishwa nyuma na Uislamu tangu karne ya 7 kwa njia ya misioni ya kisasa