Mkoa wa Rukwa
Kutoka Wikipedia
Rukwa ni moja kati ya mikoa 26 za Tanzania. Inapakana na mikoa ya Kigoma na Tabora upande wa Kaskazini, mkoa wa Mbeya upande wa mashariki, Zambia kusini na upande wa magharibi Ziwa la Tanganyika lililo mpaka na Kongo pia. Makao makuu ya mkoa ni Sumbawanga.
Eneo la mkoa ni takriban 70,000 km². Kusini mwa mkoa liko ziwa la Rukwa ambalo ni kati maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki.
[hariri] Wakazi
Kuna wakazi 1,141,743 (sensa 2002). Wilaya nne ndizo (idadi ya wakazi katika mabano): Sumbawanga Mjini (147,483), Sumbawanga Vijijini (373,080), Mpanda (412,683) na Nkansi (208,497). Kabila kuwba zaidi mkoani ndio Wafipa walioko hasa katika wilaya za Sumbawanga na Nkansi. Kati ya makabila mengine ni Wabende, Wapimbwe, Warungwa na Wakonongo katika wilaya ya Mpanda; Wamambwe-Lungu, Wawanda na Wanyamwanga katika wilaya ya Sumbawanga; kuna pia Wasukuma, Wanyamwezi na Wamassai.
[hariri] Viungo vya nje
Matokeo ya sensa 2002: en [[1]]
Makabila na lugha za Tanzania: en [[2]]
|
|
---|---|
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Iringa | Kagera | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |