Saruji
Kutoka Wikipedia
Saruji (pia: simiti, simenti) ni mata laini kama ungaunga unaotengenezwa kutokana na chokaa, udongo wa ufinyanzi, mchanga, chuma na mengine. Kwa kawaida huonekana kama unga wa rangi ya kijivu.
Hukorogwa na maji kuwa na hali kati ya ujiuji baada ya muda inaanza kuganda na kuwa imara kama jiwe.
Saruji imekuwa muhimu sana katika shughuli za ujenzi. Awali ilitumiwa kwa kushika mawe au matofari wa ukuta vikae pamoja.
Baadaye imegunduliwa ya kwamba saruji ikichanganywa na mawe madogo inaweza kumwagwa kati ya bao mbili na kuwa imara ndani yao. Kwa njia hiyo imewezekana kujenga haraka sana kwa kumwaga mchanganyiko wa saruji katika nafasi zilizoandaliwa awali. Hapa vyuma vinaingizwa ndani ya ukuta au sakafu ya saruji kwa kusudi la kuongeza uimara.