Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Wahunni - Wikipedia

Wahunni

Kutoka Wikipedia

Himaya ya Attila mnamo 450 BK
Himaya ya Attila mnamo 450 BK

Wahuni walikuwa kundi la makabila kutoka Asia ya Kati walioanza kuelekea magharibi wakati wa karne za 4 na 5 BK na kuvamia Ulaya.

Yaliyomo

[hariri] Chanzo katika Asia ya Kati

Kiasili walitokea katika maeneo kati ya Kirgizia na Mongolia ya leo. Hakuna uhakika kuhusu utamaduni na lugha yao. Wataalamu wengi huona walikuwa mchanganyiko wa makabila mbalimbali kati yao Waturuki na pia Wamongolia. Kwa jumla walikuwa wahamiaji waliofuga farasi na wanyama wengine na kuishi katika hema kwa wakati mwingi.

Sababu ya uhamisho wao haijulikani. Kuna taarafi ya ya kwamba wahamiaji wa Asia ya kati walishindwa na Wachina mnamo mwaka 352. Kwa hiyo inawezekana ya kwamba makabila yalianza kuelekea magharibi baada ya kushindwa hivyo. Wengine husema ya kwamba palikuwa na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyoongeza ugumu wa maisha na kuwasababisha kutafuta nchi mpya.

Picha hii ilichorwa katika karne ya 19 na kuonyesha jinsi gani mchoraji aliwaza vita za Wahunni
Picha hii ilichorwa katika karne ya 19 na kuonyesha jinsi gani mchoraji aliwaza vita za Wahunni

[hariri] Kufika Ulaya

Kuanzia mwaka 374 Wahunni walifika katika maeneo ya mto Volga na kushambulia amkabila ya Kigermanik waliokaa pale. Wakaendelea kuhamia magharibi na kuvamia nchi nyingi. Walioogopwa sana kwa sababu ya ukali wao na mbinu zao za kushambulia haraka. Hawakuwa na wanajeshi wa miguu bali walipanda farasi na kutumia hasa pinde na mishale. Kwa njia hiyo wakasababisha mwendo mkubwa unaoitwa "uhamisho wa mataifa" katika historia ya Ulaya kati ya karne ya 5 na karne ya sita.

[hariri] Wahunni kama chanzo cha uhamisho wa mataifa katika Ulaya

Mashambulio ya Wahunni yalisababisha makabila mengi ya Wagermanik kukimbia wakielekea magharibi vilevile na kuingia katika maeneo ya Dola la Roma. Uvamizi huu wa Wagermanik waliokuwa wakimbizi mbele ya Wahunni ulidhoofisha Dola la Roma na kuwa sababu kuu kwa mwisho wake. Kati ya Wagermanik waliokimbia walikuwa pia Wavandali walioendelea kuhamahama hadi Afrika ya Kaskazini.

[hariri] Attila kuongoza Wahunni wote

Wahunni walikuwa na udhaifu bado kwa sababu waligawanyika katika vikundi vingi.Mnamo mwaka 433 Attila alifaulu kushika utawala wa pekee. Alikuwsanya Wahunni wengi kwenye makambi makubwa katika eneo la Hungaria ya leo. Kutoka hapa walishambulia nchi jirani; hawakuwa na kusudi la kuteka nchi hizo bali kupora nchi, kuiba mifugo na vyakula na kudai pesa ili wasiendelee. Attilaa aliharibu miji ny vijiji vya nchi za Balkani na kuingia hadi Germania (Ujerumani), Gallia (Ufaransa) na Italia. Mwaka 451 alishindwa na mabaki ya jeshi la Roma pamoja na makabila ya Kigermanik katika eneo la Ufaransa ya magharibi.

[hariri] Mwisho

Baada ya kifo cha Attila watoto wake walishindana kuhusu urithi. Mmoja-mmoja walishindwa sasa na Roma ya Mashariki na Wagermanik. Wahunni walitawaynika na kupotea katika historia. Mabaki yao yaliingia katika makabila mengine.


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -