Ndege (mnyama)
Kutoka Wikipedia
Ndege ni wanyama wenye uti wa mgongo (chordata) na miguu miwili wanaozaa kwa kutaga mayai. Biolojia inawapanga katika ngeli ya aves. Ndege wameenea kote duniani kuanzia Aktiki hadi Antaktiki. Ndege mdogo huwa na sentimita 5 na ndege mkubwa ana urefu wa mita mbili na nusu.
Ndege huwa na manyoya, mdomo bila meno, mayai yenye ganda gumu, moyo wenye vyumba vinne na mifupa mipesi ambayo ni imara. Ndege walio wengi wana uwezo wa kuruka hewani na maumbile yao yanalingana na matembezi ya hewani. Ila tu aina chache zimepoteza uwezo wa kuruka kwa mfano mbuni, pengwini na ndege kadhaa za visiwani.
Aina nyingi za ndege huwa na matembezi ya kila mwaka kwa mfano Korongo husafiri kila mwaka kati ya Afrika na Ulaya.
[hariri] Aina kadhaa za ndege