Vumatiti
Kutoka Wikipedia
Vumatiti | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Vumatiti mdogo
|
||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Vumatiti ni ndege wakubwa wa jenasi kadhaa (angalia sanduku ya uainishaji) katika familia ya Ardeidae wenye domo refu na nyembamba lakini shingo fupi kuliko spishi nyingine za familia hii. Hupinda shingo yao wakiruka angani. Ndege hawa wana rangi nyeupe, nyeusi na kahawia. Vumatiti hula samaki, amfibia na wadudu wa maji. Hizi ni spishi zinazojificha ndani ya uoto. Hujenga matago yao kwa matawi juu ya( miti au) matete. Hata matago yamefichika kwa kawaida.
[hariri] Spishi za Afrika
- Botaurus stellaris, Vumatiti Mkubwa (Great Bittern)
- Ixobrychus minutus, Vumatiti Mdogo (Little Bittern)
- Ixobrychus sturmii, Vumatiti Kibete (Dwarf Bittern)
- Tigriornis leucolopha, Vumatiti-msitu (White-crested Tiger Bittern)
[hariri] Spishi za mabara mengine
- Botaurus lentiginosus (American Bittern)
- Botaurus pinnatus (South American Bittern)
- Botaurus poiciloptilus (Australasian Bittern)
- Ixobrychus cinnamomeus (Cinnamon Bittern)
- Ixobrychus eurhythmus (Schrenck's Bittern)
- Ixobrychus exilis (Least Bittern)
- Ixobrychus flavicollis (Black Bittern)
- Ixobrychus involucris (Stripe-backed Bittern)
- Ixobrychus sinensis (Yellow Bittern)
- Tigrisoma fasciatum (Fasciated Tiger Heron)
- Tigrisoma lineatum (Rufescent Tiger Heron)
- Tigrisoma mexicanum (Bare-throated Tiger Heron)
- Zonerodius heliosylus (New Guinea Tiger Heron)