Karolo Mkuu
Kutoka Wikipedia
Karolo Mkuu (Kilatini: Carolus Magnus; Kijer.: Karl der Große; Kifar.: Charlemagne) aliishi kati ya 742 hadi 814 akawa mfalme wa Wafranki na Kaizari wa Dola takatifu la Roma
Alikuwa mwana wa mfalme Pippin mfupi akarithi nusu ya milki ya babake. Akaendelea kuunganisha nchi zote za Wafranki katika Ufaransa na Ujerumani ya leo baada ya kifo cha kakake kuanzia mwaka 786. Aliendelea kuvamia na kuteka nchi ya Wasaksoni katika kaskazini ya Ujerumani.
Kwa njia ya ndoa akajipatia 774 pia taji la ufalme wa Lombardia katika Italia ya Kaskazini. Akiwa na athira kubwa katika Italia pamoja na Ufaransa na Ujerumani akapewa cheo cha Kaizari na Papa Leo III wa Roma.
Kwa njia hiyo alianzisha upya cheo cha Kaizari wa Roma katika magharibi.
Alipenda elimu akaanzisha shule kadhaa. Alipokufa 814 mtoto wake Ludoviko alirithi ufalme kutoka kwake.