Firenze
Kutoka Wikipedia
Firenze ni mji katika Italia na makao makuu ya mkoa wa Toscana. Kati ya 1865 hadi 1870 ilikuwa pia mji mkuu wa Ufalme wa Italia. Mji uko kando la mto Arno. Idadi ya wakazi ni mnano 400,000 na pamoja na rundiko la mji ni takriban 600,000.
Katika karne ya nyakati za kati Firenze ilikuwa kituo muhimu cha biashara, uchumi na utamaduni katika Ulaya. Ni kati ya miji ambako uchumi wa benki ulijitokeza.
Firenza hutajwa mara nyingi kama chanzo cha kipindi cha "Renaissance" yaani kuzaliwa upya kwa utamaduni wa kale katika Ulaya. Wakati ule ulitawaliwa na familia ya Medici. Mji umepabwa na majengo mazuri sana yanayojaa picha za kupendeza. Wasanii wengi walio muhimu katika utamaduni wa Ulaya waliishi Firenze kama vile Donatello, Botticelli, Michelangelo na Leonardo da Vinci. Pia watu kama mwanafalsafa wa kisiasa Machiavelli, mpelelezi wa Amerika Amerigo Vespucci na mwanasayansi Galileo Galilei waliishi Firenze.
[hariri] Picha
Ponte Santa Trinita Firenze.jpg
Ponte Santa Trinità (daraja la Utatu Mtakatifu) |