Medici
Kutoka Wikipedia
Medici ni jina la familia ya Firenze katika Italia iliyokuwa muhimu kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni wakati wa karne za 15 na 16 BK. Mapapa watatu wa kanisa katoliki walikuwa Wamedici pamoja na watawala mbalimbali za mji wa Firenze na watoto wao walioa au kuolewa katika familia za wafalme wa Ulaya.
Walijenga utajiri katika biashara ya kitambaa wakaendelea kuunda benki kadhaa zilizokuwa aina mpoya ya biashara wakati ule. Uwezo wao wa kiuchumi walitumia baadaye kisiasa.
Watawala na mapapa Wamedici waliajiri wasanii wengi na kugharamaia pia wataalamu hivyo wakajenga kipindi cha utamaduni wa juu cha Italia kilichong'aa kote Ulaya.
[hariri] Wamedici mashuhuri
- Salvestro de' Medici (1331 – 1388) alikuwa wa kwanza wa familia aliyetawala Firenze hadi 1382
- Giovanni di Bicci de' Medici (1360 – 1429) aliongeza utajiri wa nyumba hadi kuwa familia tajiri ya Ulaya
- Cosimo Mzee (1389 – 1464) alianzisha mfululizo wa watawala Wamdedici wa Firenze
- Lorenzo de' Medici (1449 – 1492) mtawala wa Firenze aliyetumia pesa nyingi kwa sanaa na wasanii
- Giovanni de' Medici (1475 – 1523) aliyekuwa Papa Leo X
- Giulio de' Medici (1478 – 1534) aliyekuwa Papa Klementi VII
- Cosimo I de' Medici (1519 – 1574) aliendelea kuwa mtemi wa Toskana
- Catherine de' Medici (1519 – 1589), Queen of France
- Alessandro Ottaviano de' Medici (1535 – 1605) aliyejulikana kama Papa Leo XI
- Marie de' Medici (1575 – 1642) aliyekuwa malkia wa Ufaransa
- Anna Maria Luisa de' Medici (1667 – 1743) alikuwa mtemi wa Toskana na mwisho wa familia ya Medici alieyeaga dunia bila watoto.
[hariri] Viungo vya Nje
- Outline of the history of the Medici family
- Genealogical manuscript on the house of the Medici
- Template:De icon Genealogical tree of the house of the Medici
- Galileo and the Medici Family at PBS
- Adrian Fletcher’s Paradoxplace – 3 pages of Medici portraits and history
- Medici Archive Project
Makala hiyo kuhusu "Medici" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Medici kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |