Bismuthi
Kutoka Wikipedia
Bismuthi (bisemutum; kiing. Bismuth) |
|
---|---|
|
|
Jina la Elementi | Bismuthi (bisemutum; kiing. Bismuth) |
Alama | Bi |
Namba atomia | 83 |
Mfululizo safu | Metali |
Uzani atomia | 208.980 |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 18, 5 |
Densiti | 9.78 g/cm³ |
Kiwango cha kuyeyuka | 544.7 K (271.5 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 1837 K (1564°C) |
Asilimia za ganda la dunia | 2 · 10-5 % |
Hali maada | mango |
Mengineyo | nururifu kidogo; Bismuthi tupu ina umbo la fuwele |
Bismuthi ni elementi nururifu yenye namba atomia ya 82 kwenye mfumo radidia na uzani atomia ni 209.980. Jina latokana katika lugha ya Kijerumani lakini maana hayajulikani tena.
[hariri] Tabia
Ni metali nzito na kechu yenye rangi nyeupe-nyekundu lakini inaonekana kwa rangi mbalimbali. Tabia zake hufanana na antimoni na asenia lakini si sumu vile.
Mwaka 2003 imetambuliwa kuwa Bismuthi ni nurufifu kidogo. Lakini nusumaisha yake ni takriban miaka trilioni 19 hivyo haina hatari kwa binadamu.
[hariri] Matumizi
Hutumiwa kwa madawa ya vipodozi na madawa ya kiganga. Bismuthi imechukua nafasi ya metali ya risasi katika madawa kwa sababu si sumu. Kuna pia matumizi katika teknolojia mbalimbali.
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Bismuthi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Bismuthi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |