Bara la Antaktiki
Kutoka Wikipedia
Antaktiki ni bara kwenye ncha ya kusini ya dunia. Kwa sababu ya baridi kali katika bara hii, ni bara ya pekee ambapo hawaishi binadamu wowote isipokuwa kuna wanasayansi wanaokaa kwa muda katika vituo vyao.
Takriban 98% za eneo la bara lafunikwa na theluji na barafu. Bara liko kati ya bahari za Pasifiki, Atlantiki na Bahari Hindi. Eneo lake ni kubwa kushinda Ulaya lakini hakuna mti hata mmoja.
Kuna volkeno hai moja inayotema moto barani ni mlima wa Mount Erebus.
[hariri] Viungo vya Nje
- Antarctic Place-names Commission of Bulgaria
- L.L. Ivanov et al, Topographic map of Livingston Island and Greenwich Island