Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Amerika ya Kilatini - Wikipedia

Amerika ya Kilatini

Kutoka Wikipedia

Nchi za Amerika ya Kilatini zinazotumia lugha za Kihispania, Kireno na Kifaransa. Belize imo kwa sababu ya wasemaji wengi wa Kihispania.
Nchi za Amerika ya Kilatini zinazotumia lugha za Kihispania, Kireno na Kifaransa. Belize imo kwa sababu ya wasemaji wengi wa Kihispania.

Amerika ya Kilatini ni jina la kutaja sehemu kubwa ya Amerika.

[hariri] Asili ya jina

Amerika ya Kilatini humaanisha kwa kawaida nchi za Amerika ambako lugha za Kihispania na Kireno pamoja na Kifaransa hutumiwa kama lugha rasmi au lugha ya watu wengi. Lugha hizi zote zimetokana na Kilatini na hujumlishwa kama "Lugha za Kirumi".

[hariri] Nchi za Amerika ya Kilatini

Kuna tofauti kuhusu ya namna ya kutaja nchi za Amerika ya Kilatini. Mara nyingi Amerika ya Kusini, Amerika ya Kati na Meksiko hutajwa hivyo kwa jumla. Lakini kuna nchi ndogo kama Guyana, Surinam na nchi za visiwani vya Karibi zinazotumia zaidi Kiingereza au Kiholanzi zisizo lugha za Kirumi. Nchi hizi wakati mwingini hujumlishwa pamoja ndani ya Amerika ya Kilatini lakini mara nyingi zinatazamiwa kuwa pekee kiutamaduni.

Kiutamaduni hata sehemu ya Marekani ya Kusini yenye wasemaji wengi wa Kihispania ni karibu sana na Amerika ya Kilatini. Majimbo haya ya Marekani kama Texas na Kalifornia yalikuwa sehemu za Meksiko hadi karne ya 19.

[hariri] Historia na utamaduni

Kipaumbele cha lugha za Kirumi kimetokana na historia. Baada ya Kristoforo Kolumbus nchi hizi zilikuwa koloni ama za Hispania au za Ureno hadi karne ya 19. Wakazi wengi ni watoto wa wahamiaji kutoka Ulaya au chotara kati ya wahamiaji wale na wakazi asilia.

Katika nchi kadhaa hasa Meksiko na nchi za Andes ambako wakazi Waindio wengi kidogo walibaki wanaoendelea kutumia lugha zao pamoja na Kihispania.

Dini kubwa katika Amerika ya Kilatini ni Kanisa Katoliki lililokuwa kanisa rasmi ya Hispania na Ureno.


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -