Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Andes - Wikipedia

Andes

Kutoka Wikipedia

Safu za milima ya Andes zinavyoonekana kutoka angani
Safu za milima ya Andes zinavyoonekana kutoka angani

Andes ni safu ndefu kabisa ya milima duniani. Inavuka urefu wote wa Amerika Kusini kutoka Kolombia katika kaskazini hadi Chile katika kusini upande wa magharibi wa bara hili ikiongozana na mstari wa pwani la Pasifiki. Urefu wa safu yote ni takriban 7,500 km. Milima ya juu inafikia kimo cha 6,962 m na wastani ya milima yote iko kwa 4000 m. Upana wa milima hii ni kati ya 200 km na 600 km.

Yaliyomo

[hariri] Safu za milima na nyanda za juu

Ndani ya Andes kuna hasa safu mbili zinazokwenda sambamba kandokando lakini kuna pia sehemu ambako safu zimeongezeka kuwa zaidi ya mbili. Hizi safu kuiu ni "Cordillera Oriental" (safu ya mashariki) na "Cordillera Occidental" (safu ya magharibi); kati ya safu za pembeni kuna ile ya Cordillera de la Costa (safu ya pwani) nchini Chile. Katika sehemu ya katikati safu hizi zinazunguka nyanda za juu za Altiplano za Peru na Bolivia.

[hariri] Nchi za Andes

Nchi saba za Amerika kusini zina sehemu za maeneo yao katika Andes: Kolombia, Ekuador na Venezuela katika kaskazini; Peru na Bolivia katikati, halafu Argentina na Chile katika kusini.

Licancabur, Bolivia/Chile
Licancabur, Bolivia/Chile
Llullaillaco, Chile/Argentina
Llullaillaco, Chile/Argentina
Aconcagua, Argentina
Aconcagua, Argentina
Chimborazo, Ecuador
Chimborazo, Ecuador
Alpamayo, Peru
Alpamayo, Peru
El Misti, Peru
El Misti, Peru
Pico Bolívar, Venezuela
Pico Bolívar, Venezuela


[hariri] Milima mirefu

Milima mirefu zaidi iko katika kaskazini ya Chile na Argentina, halafu katika Peru, Bolivia na Ekuador.

Mlima mrefu kabisa ni Aconcagua katika Argentina kwenye mpaka wa Chile ambao ni mlima mrefu wa Amerika yote.

  • Nevado Huascarán, 6.768 m (Peru)
  • Alpamayo, 5.947 m (Peru)
  • Nevado Yerupajá, 6.634 m (Peru)
  • Nevado Illimani, 6.483 m (Bolivia)
  • Cerro Torre, 3.133 m (Argentinia)

[hariri] Volkeno

Andes zina volkeno nyingi kwa sababu ziko sehemu ya "mviringo wa moto" unaozunguka Pasifiki yote. Bamba la Nazca linajisukuma chini ya bamba la Amerika Kusini na kusababisha kukunjwa juu kwa safu za Andes. Magma hupanda juu kwenye mstari wa kuzama kwa bamba la Nazca hulisha volkeno. Andes ni mahali pa volkeno za kimo kikubwa duniani.

  • Monte Pissis, 6,882 m (Argentina)
  • Ojos del Salado, 6,864 m (Argentina - Chile)
  • Cotopaxi, 5.897 m (Ekuador)
  • Tungurahua, 5.010 m (Ekuador)
  • Pichincha, 4.784 m (Ekuador)
  • Villarrica, 2.840 m (Chile)
  • Llullaillaco, 6.723 m (Argentinien/Chile)
  • Nevado Coropuna, 6.426 m (Peru)
  • Ubinas, 5.675 m (Peru)
  • Chimborazo, 6.310 m (Ekuador)
  • Osorno, 2.652 m (Chile)
  • Sierra Nevada de Lagunas Bravas 6.127 m (Chile/Argentina)
  • Lanín, 3.747m (Argentina)
  • Uturunco, 6.010 m (Bolivia)
  • Licancabur, 5.916 m (Bolivia/Chile)
  • Misti, 5.822 m (Peru)
  • Volkeno nyingi ndogo katika Bonde la Volkeno - (Peru)


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -