Uingereza (nchi)
Kutoka Wikipedia
|
|||||
Wito (Kifaransa): Dieu et mon droit ("Mungu na haki yangu") |
|||||
Mahali pa Uingereza (kijani cheusi) kwenye visiwa vya Britania ndani ya Ufalme wa Muungano (kijani nyeupe) pamoja na Jamhuri ya Ueire (buluu) upande wa magharibi |
|||||
Lugha | Kiingereza | ||||
Mji Mkuu | London | ||||
Mji Mkubwa | London | ||||
Eneo – jumla |
130,395 km² |
||||
Wakazi –2004 |
50.1 millioni [1] 49,138,831 [2] |
||||
Umoja wa nchi yote | 927 BK na mfalme Athelstan |
||||
Dini rasmi | Church of England (Anglikana) | ||||
Pesa | Pound sterling (£) (GBP) | ||||
Masaa | UTC / (GMT) Summer: UTC +1 (BST) |
||||
Ua la Taifa | Waridi ya Tudor (nyekundu, nyeupe) | ||||
Mtakatifu wa kitaifa | Mt George |
Uingereza ni nchi kubwa ndani ya Ufalme wa Muungano yenye wakazi milioni 50 au 83% ya wakazi wa Ufalme wote na eneo lake ni theluthi mbili ya kisiwa cha Britania.
Katika lugha ya kila siku "Uingereza" hutaja mara nyingi Ufalme wote au kisiwa.
Yaliyomo |
[hariri] Jiografia
Uingereza iko kwenye kisiwa cha Britania ambayo ni kisiwa kikubwa cha Ulaya. Imepakana na Welisi upande wa magharibi na Uskoti upande wa kaskazini. Mji Mkuu ni London. Ufaransa iko upande wa kusini ng'ambo ya Mfereji wa Kiingereza. Tangu mwaka 1994 kuna njia ya reli kwa tobwe chini ya mfereji inayounganisha Uingereza na Ufaransa.
Kati ya miji mikubwa ya Uingereza ni: London, Manchester, Birmingham, Leeds, Sheffield, Bradford na Liverpool.
Uingereza ina visiwa vingi vidogo; kikubwa ni Isle of Wight katika kusini.
[hariri] Mito ya Uingereza
- Severn(mto mrefu wa Britania)
- Thames
- Trent
- Humber
- Tyne
- Tees
- Ribble
- Ouse
- Mersey
- Dee
- Avon
[hariri] Historia
Uingereza ilikaliwa na makabila ya Wabritania wenye lugha za Kikelti na kuvamiwa na Dola la Roma katika karne ya pili BK. Ikawa sehemu ya Dola la Roma hadi karne ya tano BK. Wakati ule Waroma walipaswa kuondoa wanajeshi wao kisiwani kwa ajili ya ulinzi wa nchi za bara.
[hariri] Uvamizi wa Waanglia-Saksoni
Katika karne za 5 na 6 BK makabila ya Kigermanik walivamia kisiwa hasa Wasaksoni, Waanglia na Wadenmark. Walileta lugha zao za Kigermanik zilizochukua nafasi ya lugha ya Wabritania.
Wabritania na Waroma waliokuwa wamebaki walihamia maeneo ya kando kama Welisi au Cornwall au kuvuka mfereji wa Uingereza kwenda Britania Ndogo (Kiingereza:Brittany; Kifaransa: Bretagne).
Karne zilizofuata kisiwa kiliona madola madogo na hali ya vita. Mwaka 937 Mfalme Athelstan aliweza kuunganisha karibu eno lote la Uingereza ya leo.
[hariri] Uvamizi wa Wanormani
Mwaka 1066 wanajeshi Wanormani kutoka kaskazini ya Ufaransa walivamia Uingereza na kuteka yote chini ya mtemi William Mshindi. Wavamizi walitawala wakitumia aina ya Kifaransa. Lugha zote mbili za wananchi na za mabwana ziliendelea pamoja sambamba hadi kuwa lugha moja cha Kiingereza.
[hariri] Ufalme wa Muungano
Tangu mwaka 1601 mfalme James VI wa Uskoti alichaguliwa kuwa mfalme wa Uingereza pia. Nchi jirani zote mbili ziliendelea na mfalme mmoja hadi mwaka 1707. Mwaka ule Uingereza pamoja na Welisi na Uskoti ziliunganishwa kuwa Ufalme wa Muungano wa Britania. Tangu 1801 jina likawa Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire (United Kingdom of Great Britain and Ireland) hadi 1927 wakati sehemu kubwa ya Eire ikapata uhuru wake. Tangu 1927 Uingereza ni sehemu ya Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini (United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland).