Seli
Kutoka Wikipedia
Seli (kutoka Kilatini cellula = chumba kidogo) ni chumba kidogo ndani ya mwili wa binadamu, wanyama na mimea. Mwili wote wa kila kiumbehai hufanywa na seli. Viumbehai vidogo sana kama bakteria huwa na seli moja tu. Mwili wa mwanadamu huwa na seli trilioni 100 au 1014. Kila yai ni seli moja hivyo seli kubwa duniani ni yai la mbuni. Seli za kawaida ni ndogo sana hutazamiwa kwa kutumia hadubini.
[hariri] Muundo wa seli
Kimsingi kila seli huwa na
- kiini cha seli,
- utando wa seli (ganda la nje) na
- utegili unaojaza chumba ndani ya utando. Ndani ya utegili kuna sehemu nyingine zenye kazi mbalimbali kama ribosomu au dutuvuo (mitokondria), .