Hadubini
Kutoka Wikipedia
Hadubini (pia: darubini ya vidudu) ni kifaa cha kutazama vitu vidogo sana. Ni chombo muhimu cha sayansi kwa utafiti wa vitu ambavyo ni vidogo mno kwa jicho la kibinadamu.
Hadubini ya kawaida (hadubini maonzi) huwa na lenzi zinazokuza kiolwa kinachowekwa chini yake. Kwa kawaida kuna lenzi kadhaa zenye viwango tofauti vya kukuza. Muundo wake hufanana na darubini lakini inaangalia vitu kwa karibu ambavyo ni vidogo kimaumbile. Darubini inaangalia violwa vya mbali vinayoonekana vidogo kutokana na umbali.
Uwezo wa hadubini ya kawaida ni kukuza hadi mara 1,500.
Kwa utafiti wa vitu vidogo zaidi kuna teknolojia ya hadubini elektronia. Kifaa hiki hutumia elektroni badala ya nuru kwa utafiti wake na kuwezesha kutazama yaliyomo ya molekuli.