Darubini
Kutoka Wikipedia
Darubini (kutoka Kiajemi دوربين dorbin) ni kifaa cha kutazamia vitu ambavyo ni mbali. Kutegemeana na kusidi lake kuna aina mbalimbali:
- darubini ndogo za mkononi ni vyombo vinavyotumiwa na wapenda mazingira asilia, wavindaji, polisi na jeshi.
- darubini maonzi kubwa hutumiwa na wanafalaki kwa kutazama magimba ya angani kama jua, mwezi, nyota, sayari au kometi.
- darubini redio hutumiwa pia na wanafalaki zikikusanya mishale ya sumakuumeme zinazofaa kutupa picha za violwa vya mbali sana zisizoonekana kwa njia ya nuru ya kawaida. Zinafaa pia kuonyesha tabia za violwa vya angani vya karibu zaidi zisizoonekani wka njia ya nuru.
Darubini maonzi hutumia ama lenzi pekee au kiakisi pamoja na lenzi.
[hariri] Historia ya darubini
Darubini ya kwanza inayojulikana ilitengenezwa mwaka 1608 na Mholanzi Hans Lipperhey aliyekuwa fundi miwani. Mfano wake ulichukuliwa na kuboreshwa na mwanafalaki Mwitalia Galileo Galilei aliyeanza kuitumia mwaka 1610 kwa kuangalia nyota. Aligundua mara moja miezi ya sayari Mshtarii. Aina nyingine ya darubini ilielezwa na Mjerumani Johannes Kepler mwaka 1611.
Muundo tofauti uligunduliwa na padre Nicolaus Zucchius mwaka 1616 iliyotumia kiakisi parabola kwa kukusanya mishale ya nuru.
Katia karne zilizofuata vyombo hivi viliendelea kuboreshwa. Mtambo mpya ulipatikana katika karne ya 20 kwa kutumia mnururisho wa sumakuumeme kutoka kwa nyota iliyoendelezwa kuwa darubini redio.
[hariri] Viungo vya Nje
- http://www.eso.org/projects/owl/
- The Resolution of a Telescope
- http://www.eurocosm.com/Application/images/telescopes/525-telescope-lg.jpg
[hariri] Tazama pia
- Hadubini (au darubini ya vidudu)