Robert Mugabe
Kutoka Wikipedia
Robert Gabriel Mugabe (* 21 Februari 1924) amekuwa kiongozi wa Zimbabwe tangu 1980. Yeye ni mwenyekiti wa chama tawala cha ZANU. 1980 alikuwa waziri mkuu na 1987 rais wa nchi. Kabla ya wakati ule aliongoza upinzani wa ZANU dhidi ya serikali ya walowezi Waingereza nchini waliofuata siasa ya ubaguzi wa rangi.
Mugabe alirudiwa katika uchaguzi mbalimbali. Tangu mwaka 2000 uchaguzi hizi zimekuwa mashakani kutokana na matishio na matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani. Utawala wa Mugabe umeitwa wa kidikteta tangu mwaka 2002. Kutokana na mashataka dhidi ya serikali ya Mugabe ya kudharau haki za binadamu nchi Zimbabwe ilisimamishwa ndani ya Jumuiya ya Madola. Mugabe pamoja na mawaziri wake na viongozi wa chama chake hawaruhusiwi kusafiri kwenda nchi za Umoja wa Ulaya na Marekani.
Mwanzoni wa utawala wake Mugabe alisifiwa kujenga uchumi na sera ya elimu nchini. Zimbabwe ilikuwa nchi iliyouza vyakula vingi nje. Tangu mwanzo wa milenia mpya pamoja na mashtaki ya udikteta hali ya uchumi ulirudi nyuma. Takriban milioni mbili za raia wa Zimbabwe wameondoka nchini wakikaa kama wakimbizi Afrika Kusini.
Mugabe ametangazwa upya na chama cha ZANU kama mgombea wa urais katika uchaguzi wa 2008.