Melbourne
Kutoka Wikipedia
Melbourne ni mji mkubwa katika Australia ya kusini na mji mkuu wa jimbo la Victoria. Ina wakazi 3,720,300.
Mji uliundwa mwaka 1835 kando hori ya Port Phillip Bay ya Pasifiki. Ilikuwa haraka baada ya kupatikana dhahanu tangu 1851. Imekuwa kitovu cha kiuchumi, kiutamaduni na kimichezo. Katika karne ya 19 ilikuwa mji mkubwa wa Australia na pia mji mkuu wa taifa hadi uhamisho wa bunge kwenda Canberra mwaka 1901.
Siku hizi kuna wakazi kutoka nchi nyingi waliohamia Australia na kukaa mjini. Robo ya wakazi wake walizaliwa nje kuna watu kutoka nchi 233 na lugha 180 zinajadiliwa mjini hata kama theluthi mbili za wakazi hutumia Kiingereza kwao nyumbani.