Boroni
Kutoka Wikipedia
Boroni ni elementi ya kikemia yenye namba atomia 5 kwenye mfumo radidia na uzani atomia 10.811. Alama yake ni B.
Yaliyomo |
[hariri] Tabia
Boroni ni nusumetali au metaloidi ina valensi tatu. Elementi pekee yake haipatikani katika mazingira asilia duniani ila tu katika kampaundi kama vile borasi (Na2B4O7·10H2O ).
[hariri] Umbo hobela au la fuwele
Inapotapaswa kutoka kwa kampaundi zake hupatikana katika umbo hobela kama unga wa rangi kahawia au la fuwele nyeusi na ngumu isiyohami umeme. Boroni ni dutu ngumu duniani baada ya almasi na kati ya elementi zote ni imara dhidi ya nguvu ya mvuto.
[hariri] Matumizi kiteknolojia
Matumizi ya boroni ni katika teknolojia ya kihami na katika madawa ya kupausha au kung'arisha. Inatumiwa pia kama nyongeza katika aloy kwa ajili ya sehemu za eropleni zinazotakiwa imara ma nyepesi.
[hariri] Nafasi ya kibiolojia
Kwa kiasi ndogondogo boroni ina kazi katika miili ya wanyama isipokuwa bado haijaeleweka ni kazi gani isipokuwa imeonekana ni muhimu.
Makala hiyo kuhusu "Boroni" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Boroni kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |