Pentekoste
Kutoka Wikipedia
Pentekoste ni sikukuu ya kikristo ya kukumbuka umwagaji wa Roho Mtakatifu juu ya mitume au wanafunzi ya Yesu Kristo na kuanzishwa kwa kanisa la kikristo. Husheherekewa jumapili ya 7 baada ya Pasaka.
Yaliyomo |
[hariri] Jina
Jina la "Pentekoste" ni la asili ya Kigiriki "πεντηκοστή" [ἡμέρα] (pentekostē [hēmera]) yaani (siku ya) hamsini. Neno hili ni namba 50 kwa kumaanisha siku ya 50 baada ya Pasaka au ufufuo wa Yesu.
[hariri] Pentekoste ya Kwanza
Maelezo juu ya Pentekoste ya kwanza hupatikana katika sura ya pili ya kitabu cha Matendo ya Mitume cha Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo. Luka asimulia jinsi wanafunzi wa Yesu walikutana katika mji wa Yerusalemu siku ile ya "pentekoste" na kupokea kipaji cha Roho Mtakatifu. Baadaye walitoka nje wakianza mara ya kwanza kuhubiri habari za Yesu Kristo mbele ya watu wengi pamoja na wageni kutoka nchi nyingi. Kufuatana na taarifa watu wengi walibatizwa kwa jina la Yesu na takriban 3,000 waliongezeka katika kile kikundi siku hiyo.
[hariri] Pentekoste ya Kikristo na Shavuot ya Kiyahudi
Ile siku inatajwa kama "siku ya hamsini" iliyokuwa sikukuu ya Kiyahudi siku ya hamsini baada ya Pasaka ya Kiyahudi. Sikukuu hii husheherekewa na Wayahudi kama "shavuot" jinsi ilivyoamriwa katika kitabu cha Mambo ya Walawi 23:16. Kwa hiyo inawezakana kusema ya kwamba baada ya kifo na ufufuo wa Yesu wanafunzi wake -ambao walikuwa Wayahudi wote- walikutana kwenye sikukuu ya kiyahudi ya Shavuot wakikutana na Wayahudi kutoka nchi mbalimbali waliotembelea Yerusalemu kwenye nafasi ya sikukuu ile.
Tangu kuachana kwa kalenda ya Kikristo na kalenda ya Kiyahudi sikukuu zile kwa kawaida hazifiki siku ileile tena.
[hariri] Tarehe ya Pentekoste
Katika makanisa yanayofuata kalenda ya Gregori Pentekoste itasheherekwa kwenye tareke zifuatazo:
- 2006: 4 Juni
- 2007: 27 Mei
- 2008: 11 Mei
- 2009: 31 Mei
- 2010: 23 Mei
- 2011: 12 Juni
- 2012: 27 Mei
- 2013: 19 Mei
- 2014: 8 Juni
- 2015: 24 Mei
- 2016: 15 Mei
- 2017: 4 Juni
- 2018: 20 Mei
- 2019: 9 Juni
- 2020: 31 Mei
Makanisa ya Kiorthodoksi yanayofuata kalenda ya Juliasi huwa na tarehe tofauti.