Pasaka
Kutoka Wikipedia
Pasaka ni jina la sikukuu muhimu katika dini za Uyahudi na Ukristo. Jina la Pasaka limetokana na neno la Kiebrania "פסח" (tamka: pasakh).
- Pasaka ya Kiyahudi ni sikukuu ya kumbukumbu kwa kutoka kwa Wanaisraeli kutoka Misri wakati wa Musa mnamo miaka 1200 KK.
- Pasaka ya Kikristo ni sikukuu ya kukumbuka kufufuka kwake Yesu Kristo siku ya tatu baada ya kusulibiwa kwake. Inahesabiwa kuwa sikukuu muhimu kabisa katika Ukristo.
Taarifa za Agano Jipya zinatoa habari ya kuwa kifo na kufufuka kwa Yesu yametokea wakati wa sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi. Kwa hiyo jina la sikukuu hiyo imeendelea kutumikwa kwa ajili ya sherehe ya kikristo.
[hariri] Maneno kwa ajili ya Pasaka ya Kiyahudi na Pasaka ya Kikristo katika lugha mbalimbali (mifano)
Katika lugha nyingi asili hii bado inaonekana ingawa mara nyingi umbo la neno ni tofauti kidogo. Jina la sikukuu ya Kiyahudi linapatikana kwa umbo mbalimbali. Siku hizi mara nyingi umbo la neno la Kiebrania limetumika lakini desturi katika lugha hizo inaonyesha pia umbo linalofanana zaidi na neno kwa ajili ya sherehe ya kikristo. Lugha
Lugha | Jina la Pasaka ya Kiyahudi | Jina la Pasaka ya Kikristo |
---|---|---|
Kifaransa | Pessah | Paque; Les Paques |
Kihispania | pascua | pascua |
Kiitalia | Pasqua ebraica; Pesach; Pesah | Pasqua |
Kipoland | Pesach | Wielkanoc; Pascha |
Kirusi | Пасха; Песах (pas-kha; pesakh) | Пасха (pas-kha) |
Kigiriki | Πάσχα (pas-kha) | Πάσχα (pas-kha) |
Kidenmark | Pesach | Påske |
Kinorway | Pesah | Påske |
Kisweden | Pesach;Påsk | Påsk |
Kiholanzi | Pesach | Pasen |
Kijerumani | Passah | Ostern |
Kiingereza | Passover | Easter |
Kiajemi | پسح |
پاک |
Makala hiyo kuhusu "Pasaka" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Pasaka kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |