Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Kitabu cha Ezra - Wikipedia

Kitabu cha Ezra

Kutoka Wikipedia

Ingawa Ezekieli alifanya kazi nzuri wakati wa uhamisho wa Babeli, nabii mwingine alitumwa mwaka 550 hivi K.K. kuwatia moyo Wayahudi wenzake huko Babeli kwamba Mungu atawarudisha kwao (Is 40:1-11).

Hivyo akawafanya watamani kurudi badala ya kukwama katika kujitafutia maendeleo ya uchumi.

Hatujui jina lake, lakini tunamuita Isaya II kwa kuwa maandiko yake yamepangwa katika kitabu cha Isaya (40-55): sehemu hiyo inaitwa pia kitabu cha faraja ya Israeli.

Katika sura hizo mna mashairi manne (Is 42:1-4; 49:1-6; 50:4-9; 52:13-53:12) kuhusu mtumishi mteswa wa YHWH ambayo ndiyo utabiri bora juu ya Yesu.

Utabiri wa Isaya II ulitimia mwaka 538 K.K. ambapo mfalme Koreshi wa Uajemi, mwaka mmoja baada ya kuteka Babeli, aliwaruhusu Wayahudi warudi kwao pamoja na vitu vilivyotekwa nyara toka hekalu la Yerusalemu.

Ingawa waliorudi hawakuwa wengi, wakawa mwanzo mpya wa taifa la Mungu: walimuabudu kwa bidii katika hekalu jipya ingawa dogo (Ezra 3:10-13), walijipatia usalama kwa kujenga tena kuta za Yerusalemu (Neh 4:13-23; 12:27) na walijitenga kabisa na Wapagani (Ezra 9-10; Neh 9-10).

Habari hizo zinapatikana hasa katika vitabu vya Ezra na Nehemia, mfululizo wa vile vya Mambo ya Nyakati.

Waandishi wa vitabu hivyo vinne waliishi miaka mia hivi baadaye: ndiyo sababu walichanganya habari za hao watu wawili ambao walifanya kazi, wa kwanza upande wa dini, wa pili upande wa siasa, labda kwa nyakati tofauti.

Nehemia alipokuwa liwali wa mkoa wa Yuda wakazi walikuwa hamsini elfu tu, na eneo lao lilikuwa dogo sana.

Kuhani Ezra anasifiwa zaidi kutokana na mchango wake mkubwa katika kulipatia taifa teule sura ya kudumu, kama watu wanaoambatana kabisa na Torati, ambayo toleo lake la mwisho lilipitishwa na mfalme wa Uajemi kuwa sheria kuu ya Wayahudi (Ezra 7:1-28).

Hivyo dini yao ikawa “dini ya kitabu” hata leo.

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Maamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia Esta Tobit Yuditi Esta Yobu Zaburi Methali Mhubiri Wimbo Ulio Bora Isaya Yeremia Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki

Image:WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Kitabu cha Ezra" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Kitabu cha Ezra kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -