Iodini
Kutoka Wikipedia
Iodini (Iodium) |
|
---|---|
|
|
Jina la Elementi | Iodini (Iodium) |
Alama | I |
Namba atomia | 53 |
Mfululizo safu | Halojeni |
Uzani atomia | 126.904 |
Valensi | 2, 8, 18, 18, 7 |
Kiwango cha kuyeyuka | 386.85 K (113.7 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 457.4 K (184.3 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 6 · 106 % |
Hali maada | mango |
Iodini (kut. Kigiriki "Iodes" (ιώο-ειδης) "rangi ya dhambarau" kutokana na mvuke) ni elementi yenye namba atomia 53 katika mfumo radidia maana yake kiini atomia chake kina protoni 53. Uzani atomia ni 126.904 na alama yake ni I. Ni elementi ya nne katika safu ya halojeni.
Yaliyomo |
[hariri] Tabia
Katika hali sanifu ni mango ya fuwele yenye rangi nyeusi-kijivu. Huanza kuvukamanga kuwa gesi kwa halijoto ya chumbani tayari. Kupata iodini kiowevu inawezekana kwa kuikanza haraka hadi kufikia kiwango cha kuyeyuka cha 113.7 °C.
[hariri] Upatikanaji
Iodini yapatikana kwa wingi katika maji ya bahari pia katika madini mbalimbali.
[hariri] Iodini na tezi ya shingo
Mwili wa kibinadamu huhitaji iodini; kwa kawaida viwwango vya kutosha hupatikana katika chakula cha kawaida. Isipokuwa katika maeneo kadhaa hasa mlimani uhaba wa iodini asilia husababisha magonjwa kama tezi ya shingo.
[hariri] Matumizi
Matumizi yake ni katika madawa (hasa antiseptika), viungo vya chakula, rangi na kemia za kusafisha picha.
Iodini katika maji ni dawa antiseptika inayozuia maambukizo wa vidonda.