Waviking
Kutoka Wikipedia
Waviking ni jina la kujumlisha makundi ya watu wa mataifa ya Kigermanik katika Ulaya ya Kaskazini walioonekana kwa majirani kama wafanyabiashara na pia maharamia wa bahari.
Asili yao ilikuwa katika Skandinavia ya Kaskazini na kusini wakatumia jahazi ndogo wakavuka nazo Bahari ya Kaskazini, Bahari ya Baltiki na kuingia pia barani kupitia mito ya Ulaya hadi Mediteranea.
Mara nyingi walishambulia tu miji na vijiji vya pwani wakipora mali na kurudi kwao.
Palikuwa pia na vipindi ambako Waviking walifaulu kuteka eneo fulani na kukaa huko. Walifika Uingereza, Uskoti, Ufaransa, Hispania, Urusi hadi Bizanti na Sisilia.
Katika Uingereza, Ufaransa ya Kaskazini na Italia ya Kusini walianzisha makazi wakitawala maeneo huko kwa muda. Huko walijulikana pia kwa majina kama Wanormani au Rus na Rus walikuwa asili ya jina la Urusi.
Walivuka pia Atlantiki na kufika Greenland na Kanada.
Walihofiwa mara nyingi kama majambazi wakali lakini walitafutwa pia kama wanajeshi wa kukodi.
Inaaminiwa ya kwamba waliondoka kwao kwa sababu hali ya hewa ilileta njaa na uhaba wa ardhi ya kulima na pia kwa sababu utajiri wa nchi za kusini iliwavuta vijana wao.
[hariri] Viungo vya Nje
- BBC: History of Vikings
- Borg Viking museum, Norway
- The Viking Network
- Ibn Fadlan and the Rusiyyah, by James E. Montgomery, with full translation of Ibn Fadlan
Makala hiyo kuhusu "Waviking" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Waviking kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |