Treni
Kutoka Wikipedia
Treni (kutoka Kiing. train) ni chombo cha usafiri kwenye reli. Treni inamaanisha jumla ya mabehewa inayovutwa au kusukumwa na injini kwenye njia ya reli. Kwa lugha nyingine treni huitwa pia gari la moshi.
Mabehewa haya yanaweza kubeba watu au mizigo hivyo kuna tofauti kati ya treni ya abiria na treni ya mizigo.
Mahali ambako treni inasimama na kupokea abiria au mizigo huitwa kituo cha reli.
Makala hiyo kuhusu "Treni" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Treni kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |