Theodosius Mkuu
Kutoka Wikipedia
Flavius Theodosius (11 Januari, 347 – 17 Januari, 395) alikuwa Kaizari wa Dola la Roma kuanzia 15 Mei, 392 hadi kifo chake. Kabla hajatawala dola zima, alikuwa Kaizari upande wa Mashariki kuanzia Agosti 378. Upande wa Mashariki alimfuata Valens. Theodosius alikuwa Kaizari wa mwisho aliyetawala dola zima la Roma. Wana wake wawili walishiriki utawala, Honorius upande wa Magharibi, na Arcadius upande wa Mashariki.