Palau
Kutoka Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: | |||||
Wimbo wa taifa: Belau loba klisiich er a kelulul | |||||
Mji mkuu | Melekeok1 |
||||
Mji mkubwa nchini | Koror | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza, Kipalauan, Kijapani (kisiwani Angaur) | ||||
Serikali | Jamhuri inayoshirikiana na Marekani Tommy Remengesau |
||||
Uhuru Tarehe |
1 Oktoba 1994 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
459 km² (ya 195) -- |
||||
Idadi ya watu - Julai 2005 kadirio - Msongamano wa watu |
19,907 (ya 217) 43/km² (ya 155) |
||||
Fedha | US Dollar (USD ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+9) (UTC) |
||||
Intaneti TLD | .pw | ||||
Kodi ya simu | +680 |
||||
1 Tar. 7 Oktoba 2006 ofisi za serikali zilihamia Melekeok kutoka Koror mji mkuu wa awali. 2 Jumla la pato la taifa pamoja na msaada wa Marekani (2001) |
Palau ni nchi ya visiwani ya Mikronesia katika Bahari ya Pasifiki. Iko takriban km 500 upande wa mashariki wa Ufilipino. Jumla kuna visiwa 250 hadi 350 na idadi inategemea namna gani matazamaji anapendelea kuhesabu sehemu ya nchi kavu kuwa kisiwa kufuatana na ukubwa au udogo wake. Visiwa tisa vimekaliwa na watu na kisiwa kikubwa chenye km² 331 ni Babelthuap.
Hadi 1994 ilikuwa nchi lindwa chini ya Marekani kwa niaba ya Umoja wa Mataifa. Marekani inaendelea kuwajikiba kwa mambo ya kijeshi kufuatan na mkataba uliofanywa baada ya uhuru.
Mji mkuu ni Melekeok kwenye kisiwa cha Babelthuap.