Nyama
Kutoka Wikipedia
Nyama ni sehemu za mwili wa wanyama zinazoliwa kama chakula.
Kwa watu wengi nyama ni chakula muhimu kwa sababu ina protini nyingi ndani yake pamoja na mafuta. Nyama huliwa baada ya kuipika au kukaanga. Kuna sehemu za dunia ambako watu wamezoea kula nyama bichi wakiteua sehemu lainilaini kwa mfano nyama ya kusagwa au maini.
[hariri] Uchumi wa nyama
Gharama ya nyama ni kubwa kushinda chakula cha mboga kwa sababu kiuchumi nyama ni mboga uliobadilishwa umbo. Njia yake ni wanayama kula majani na majani haya yakikuza mnyama huwa nyama baada ya kuchinja. Kwa njia hiyo kilogramu moja cha protini ya nyama huhitaji kilogramu 5 hadi 10 protini ya mboga kama lisha ya wanyama. Kwa lugha nyingine ekari zinazolisha wanyama ya kushibisha watu 100 zinaweza kulisha watu 500 hadi 1,000 kwa njia ya nafaka au maharagwe n.k.
Katika mazingira asilia hii si tatizo kubwa kwa sababu maeneo yabisi hayakufaa kwa kilimo lakini wafugaji wahamiaji waliweza kuzunguka hapa na wanyama wao ilhali nchi yenye mvua na rutba ilitumiwa kwa kilimo cha mimea ya kulisha watu.
Kilimo cha kisasa kimebadilisha muundo huu kwa sababu sehemu kubwa ya mavuno hutumiwa kwa lishe ya wanyama. Tatizo lake linaonekana pale ambako nchi tajiri kama Marekani au Ulaya zinanunua nafaka au maharagwe kote duniani kama lishe ya wanyama wao. Kwa njia hii wanaweza kupandisha bei ya vyakula hivi na wakazi maskini wanaona bei ya vyakula zinapanda kushinda uwezo wao.
Makala hiyo kuhusu "Nyama" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Nyama kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |