Karl von Frisch
Kutoka Wikipedia
Karl von Frisch (20 Novemba, 1886 – 12 Juni, 1982) alikuwa mwanazuolojia kutoka nchi ya Austria lakini hasa alifanya kazi nchini Ujerumani. Hasa alichunguza tabia za samaki na za nyuki. Mwaka wa 1973, pamoja na Konrad Lorenz na Nikolaas Tinbergen alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.