Hispaniola
Kutoka Wikipedia
Hispaniola (Kihisp. La Española" = "cha Kihispania") ni kisiwa kikubwa cha pili katika Karibi kikiwa na eneo la 74,700 km². Iko kati ya Kuba upande wa magharibi na Puerto Rico upande wa mashariki. Hispaniola huhesabiwa kati ya visiwa vya Antili Kubwa.
Kisiwani kuna nchi mbili za Haiti na Jamhuri ya Dominika.
Nchi | Wakazi (2005-07-01 kadirio) |
Eneo (km²) |
Msongamano wa watu(kwa km²) |
---|---|---|---|
Haiti | 8,528,000 | 27,750 | 255 |
Jamhuri ya Dominika | 8,895,000 | 48,730 | 179 |
Kisiwa chote | 17,423,000 | 76,480 | 206 |