Kuba
Kutoka Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Kihispania: Patria o Muerte („Taifa au mauti“)[1] |
|||||
Wimbo wa taifa: "La Bayamesa" ("Wimbo la Bayamo") | |||||
Mji mkuu | Havana |
||||
Mji mkubwa nchini | Havana | ||||
Lugha rasmi | Kihispania | ||||
Serikali
Rais wa Halmashauri ya Dola
|
Jamhuri ya kijamii[2] Raul Castro |
||||
Uhuru Kutoka Hispania tangazo la Jamhuri ya Kuba tarehe inayokumbukwa nchini Kuba |
10 Oktoba 1868 20 Mei 1902 1 Januari 1959 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
110,861 km² (ya 105) negligible |
||||
Idadi ya watu - 2006 kadirio - 2002 sensa - Msongamano wa watu |
11,382,820 (ya 73) 11,177,743 102/km² (ya 97) |
||||
Fedha | Peso (CUC ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
EST (UTC-5) (Starts April 1, end date varies) (UTC-4) |
||||
Intaneti TLD | .cu | ||||
Kodi ya simu | +53 |
Kuba (pia: Kyuba, Cuba) ni nchi ya kisiwani katika Bahari ya Karibi kusini ya Marekani. Nchi inajumuisha kisiwa kikuu cha Kuba ambacho ni kisiwa kikubwa cha Antili Kubwa) pamoja na kisiwa cha Isla de Pinos na visiwa vingi vidogo vingine.
Kuba ni nchi kubwa kati ya nchi za Karibi yenye wakazi wengi. Utamaduni wake unaonyesha tabia za historia yake kama koloni ya Hispania ya miaka mingi pia ya wakazi wenye asili katika watumwa kutoka Afrika na kuwa jirani na Marekani.
Hali ya hewa ni ya kitropiki. Kisiwa hupigwa mara kwa mara na dhoruba kali aina za tufani.
Kuba ilikuwa koloni ya Hispania hadi 1898. Wakati ule Marekani iliingilia kati katika uasi wa Wakuba wa kupigania uhuru. Wahispania wakalazimishwa kuondoka baada ya Vita ya Marekani dhidi Hispania. Baadaye Kuba ilikuwa chini ya usimamizi wa kimarekani hadi 1934. Hadi leo kuna mabaki ya kipindi hiki ni kituo cha kijeshi cha Marekani cha Guantanamo Bay.
Mwaka 1959 kikundi cha wanamapinduzi pamoja na Fidel Castro waliteka mji mkuu wa Havana na kuanzisha serikali ya ujamaa. Baada ya kupingwa na Marekani Castro alitafuta ushirikiano na usaidizi kutoka Urusi wa kikomunsti. Castro alitangaza siasa ya kikomunisti akaendelea kutawala bila uchaguzi huru.
Makala hiyo kuhusu "Kuba" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Kuba kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |