Empire State Building
Kutoka Wikipedia
Empire State Building ni nyumba ya maghorofa mashuhuri mjini New York (Marekani) yenye umbo la mnara. Ilikuwa jengo ndefu la dunia kwa muda wa miaka 40 tangu ukamilifu wake mwaka 1931 hadi 1972 ambako minara ya World Trade Center ilijengwa mjini New York pia. Tangu kuharibiwa kwa minara hii kwenye shambulio la 11 Septemba 2001 imekuwa jengo kubwa mjini.
Ujenzi wa Empire State Building ilianza mwaka 1930. Katika muda mfupi wa mwaka mmoja na siku 45 yaani siku 410 pekee jengo lilikamilishwa. Wakati wake ilihesabiwa kati ya maajabu ya dunia ya kisasa.
Kimo chake ni mita 381, pamoha na antena juu yake ni mita 448.7.
Yaliyomo |
[hariri] Takwimu kadhaa za Empire State Building
Katika jengo hili kuna
- feleji tani 55,000 kwa kiunzi chake
- matofali milioni 10
- nyaya za umeme kilomita 760
- mabomba ya maji kilomita 96
- nyaya za simu kilomita 5600
- madirisha 6379
- ofisi 6,000 kwa wapangaji 850
- eneo la mita za mraba 715,000 za ofisi
- uzani wa jumla tani 331,000
- vyoo zaidi ya 1100
- nyanyu (lifti) 73
- ghorofa 102
- ngazi 1860 kuanzia barabara hadi kilele
[hariri] Jengo katika filamu
Empire State Building imeonekana katika filamu mbalimbali kwa mfano:
- King Kong
- James Bond
- Independence Day
- Love Affair
- SpongeBob
[hariri] Ajali
Baada ya watu kujiua kwa kuruka kutoka kilele fensi ilijengwa ya kuzungusha kilele amabako watalii wanaweza kutoka nje na kutazama mji.
Mwaka 1945 ndege ya kijeshi ya B-25 iligonga mnara kutokana na kosa la rubani wakati mawingu yalikuwa chini sana.
[hariri] Viungo vya Nje
- Tovuti rasmi ya Empire State Building
- Picha za Lewis Wickers Hine zinazoonyesha ujenzi
- Toleo maalumu ya New York Times kwa sikukuu ya miaka 75 za kufunguliwa kwa jengo 23 Aprili 2006