Bahari ya Kaspi
Kutoka Wikipedia
Bahari ya Kaspi (pia Bahari ya Qazwin- Kiajemi دريا خزر "darya khazar"; Kirusi Каспийское море "kaspiiskoye more") ni ziwa kubwa kabisa duniani lenye eno la 371,000 km² na mjao wa 78,200 km³. Liko kati ya Azerbaijan, Urusi, Kazakhstan, Turkmenistan na Uajemi.
Kimo chake mkubwa ni 1,025 m. Huitwa "bahari" kwa sababu maji yake ni ya chumvi ingawa si kali sana kama ya bahari yenyewe.
[hariri] Maji ya chumvi
Upande wa kaskazini inaingia mito miwili mikubwa ya Volga na Ural. Inasababisha kiasi kidogo cha chumvi upande huo wa kaskazini. Asilimia ya chumvi huonegezeka kuelekea kusini.
[hariri] Madini
Chini ya bahari kuna akiba kubwa za mafuta ya petroli na gesi hasa karibu na Baku. Katika hori ya Kara-Bogas chumvi hulimwa.