Yen
Kutoka Wikipedia
Yen ni pesa nchini Japani. Alama yake ya kimataifa ni ¥ lakini Japani penyewe huandikwa 円. Yen imekuwa pesa inayotumiwa sana duniani baada ya dolar na euro.
Pesa hii ilianzishwa mwaka 1871 na serikali ya Meiji ikifuata mifano ya pesa za Ulaya. Mwanzoni ililinganishwa na gramu 1.5 za dhahabu.
Thamani ya pesa ilishuka wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia na baada ya vita kiwango chake kwa dollar ya Marekani kiliweka kwa ¥360 kwa US$1. Mwaka 2008 ilikuwa ¥104 kwa US$1.
Tangu kuimarika kwa uchumi wa Japani Yen imekuwa pesa muhimu duniani.
Kuna noti za Yen 1,000, 2,000, 5,000 na 10,000.
Makala hiyo kuhusu "Yen" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Yen kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |