Xenoni
Kutoka Wikipedia
Xenoni |
|
---|---|
|
|
Jina la Elementi | Xenoni |
Alama | Xe |
Namba atomia | 54 |
Mfululizo safu | Gesi adimu |
Uzani atomia | 131.293 |
Kiwango cha kuyeyuka | 161.4 K (-111.7 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 165.03 K (-108.12°C) |
Asilimia za ganda la dunia | 2 · 10-9 % |
Hali maada | gesi |
Xenoni (pia: zenoni; kut. kigiriki ξένος ksenos “kigeni” kwa sababu wafumbuzi wa kwanza waliikuta mahali wasipoitegemea) ni elementi yenye namba atomia 54 kwenye mfumo radidia na uzani wa atomi 131.293. Alama yake ni Xe.
[hariri] Tabia
Ni gesi adimu inayopatikana katika angahewa haina rangi wala herufu. Kama gesi adimu zote ni bwete na kutomenyuka kirahisi na kitu kingine;
[hariri] Matumizi
Matumizi yake ni hasa katika aina mbalimbali za taa kwa sababu inasaidia balbu kuwa na mwanga mkali zaidi. Magari ya kisasa mara nyingi hutumia balbu za Xenoni zinatotoa mwanga mkali kwa matumizi madogo ya umeme.
Xenoni hutumiwa pia kwa vyombo vya angani kama kisukumaji. Kama gesi bwete haimenyuki na tangi na mapipa; kwa kanieneo kubwa hukaa thabiti kama kiowevu hadi halijoto ya chumbani; inageuzwa rahisi kuwa tena gesi kwa ajili ya injini.
Makala hiyo kuhusu "Xenoni" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Xenoni kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |