Stuttgart
Kutoka Wikipedia
Nembo | Ramani |
---|---|
Stuttgart ni mji mkuu wa jimbo la Baden-Württemberg nchini Ujerumani mwenye wakazi 590,000. Mji uko katika bonde kando la mto Neckar.
Stuttgart ni mji mkubwa wa sita wa Ujerumani na kitovu cha kiuchumi cha Ujerumani kusini-magharibi. Makampuni makubwa kama vile DaimlerChrysler, Porsche, Bosch, Hewlett-Packard, Kodak na IBM yana makao makuu yao kwa ajili ya Ujerumani au hata dunia nzima hapa Stuttgart.
[hariri] Historia
Wakati wa Roma ya Kale palikuwa na boma la Kiroma katika eneo la Stuttgart. Mji mwenyewe uliundwa mnamo mwaka 950 kama kituo cha kufuga farasi cha mtemi wa Swabia.
Tangu mwaka 1300 mji umekuwa mji mkuu wa watemi wa Württemberg walioendelea kujipatia cheo cha kifalme wakati wa vita za Napoleoni. Hivyo Stuttgart ikawa mji mkuu wa Ufalme wa Württemberg kuanzia 1805 hadi 1918. Baada ya mapinduzi wa 1918 Stuttgart ilikuwa mji mkuu wa jimbo la Württemberg na tangu 1952 wa Baden-Württemberg.
Mwaka 2006 Stuttgart ilikuwa mahali pa michezo katika mashindano ya soka duniani.