Shirika la Afya Duniani
Kutoka Wikipedia
Shirika la Afya Duniani (Kiing.World Health Organization - WHO) ni ni kitengo cha Umoja wa Mataifa. Inashughulika habari za afya ya umma ikilenga kuunganisha juhudi za kitaifa za kupambana na magonjwa na kujenga afya.
Kisheria WHO ni shirika lenye madola wanachama 193.
Kati ya shughuli muhimu za WHO ni progframu za kupambana na magonjwa yanayoathiri watu wengi kama vile Malaria, Ukimwi au SARS.
WHO inaratibu mipango ya kutengeneza na kusambaza madawa ya kinga. Inaratibu pia miradi ya chanjo za kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Makao makuu ya WHO yapo Geneva (Uswisi). Kuna ofisi sita za kikanda kama zifuatazo:
- Brazzaville (kanda la Afrika)
- Washington D.C. (kanda la Amerika)
- New Delhi (Rkanda la Asia ya Kusini Mashariki)
- Kopenhagen (kanda la Ulaya)
- Kairo (kanda la Mediteranea ya mashariki)
- Manila (landa la Pasifiki ya magharibi)