Herbert Brown
Kutoka Wikipedia
Herbert Brown (22 Mei, 1912 – 19 Desemba, 2004) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Marekani. Alizaliwa nchini Ukraine kwa jina la Herbert Brovarnik. Hasa alichunguza misombo mbalimbali. Mwaka wa 1979, pamoja na Georg Wittig alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.