Gustav Hertz
Kutoka Wikipedia
Gustav Ludwig Hertz (22 Julai, 1887 – 30 Oktoba, 1975) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa alichunguza sifa za atomu. Pia alivumbua njia fulani ya kutenganisha isotopu. Mwaka wa 1925, pamoja na James Franck alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.