George W. Bush
Kutoka Wikipedia
George W. Bush (* 6 Julai, 1946) amekuwa rais wa Marekani tangu mwaka 2001. Yeye ni mwenyeji wa jimbo la Texas alipokuwa gavana kabla ya kugombea uraisi.
George W. Bush ni mwana wa rais mstaafu George H. Bush aliyetawala Marekani kati ya 1989 - 1993. George W. amemwoa Laura Bush wana mabinti mawili.
[hariri] Early years
Bush alizaliwa katika jimbo la Connecticut akafuata elimu yake hadi chuo kikuu cha Yale. Hakushiriki katika vita ya Vietnam lakini alijiandikisha kati ya wanamigambo wa jimbo la Texas.
Mwaka 2000 aligombea urais kwa chama cha Republican. Alishinda kufuatana na azimio la mahakama kuu kwa sababu kura ya jimbo la Florida haikueleweka vizuri na kwa jumla kura zake zilikuwa karibu sawa na zile za mpinzani wake Al Gore.
Mwaka 2004 Bush alirudishwa kama rais kwa awamu ya pili na ya mwisho.
Vipindi viwili vya Bush viliathiriwa sana na mashambulio ya 11 Septemba 2001. Baada ya shambulio hili la Al Qaida Bush aliamuru vita dhidi ya Afghanistan ambako wagaidi wa Al Qaida walikuwa na kimbilio.
Mwaka uliofuata Bush aliuamua kwa sababu zisizoeleweka vema kushambulia pia Iraq ingawa Iraq haikushiriki katika mashambulio ya 11 Septemba wala kuwa na uhusiano na Al Qaida.
Mwanzoni Marekani pamoja namsaada wa Uingereza ilifaulu vema kushinda jeshi la Iraq na kumpindua dikteta Saddam Hussein. Lakini ushindi huu uligeukia kuwa vita ndefu ya wanamigambo wa Iraqi dhidi ya Marekani. Watu wenmgi waliendelea kufa na vita hii ya kuendelea iliharibu sifa za Bush.