Gabriel García Márquez
Kutoka Wikipedia
Gabriel García Márquez (amezaliwa 6 Machi, 1928) ni mwandishi kutoka nchi ya Kolombia na kufanya kazi kama mwandishi wa habari katika nchi mbalimbali za Amerika na Ulaya. Anajulikana hasa kwa riwaya zake, kwa mfano "Upendo wakati wa Kipindupindu" (kwa Kihispania El amor en los tiempos del cólera) iliyotolewa mwaka wa 1985. Mwaka wa 1982 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.