Chokoleti
Kutoka Wikipedia
Chokoleti ni pipi au chakula kitamu kinachotengezewa kwa kutumia kakao, sukari na mafuta. Jina latumiwa pia kwa kinywaji cha kakao.
[hariri] Historia ya chokoleti
Asili yake ni kinywaji wa watu wa Mexiko wa kale waliochemsha unga la kakao katika maji pamoja na viungo. Wahispania waliikuta kwa Azteki na kuipeleka Ulaya. Wakitumia hapa jina la Kiazteki "xocolātl" lenya maana ya "maji chungu".
Katika Ulaya ilitumiwa muda mrefu kama kinywaji na wakati wa karne ya 19 Wajerumani walianza kutengeneza pipi jinsi inavyojulikana leo.
Chokoleti huyeyuka haraka kwa sentigrefi 40-50 hivyo ni rahisi kuifinga kwa maumbo mbalimbali.
[hariri] Hatua za kutengeneza chokoleti
- Chanzo ni mbegu za kakao.
- Hizi zinakaushwa, kukaangwa na kusagwa. Mbegu zinazosagwa zina kiasi kikubwa cha mafuta ndani yake.
- Yote yakandamizwa na mafuta ya kakao yanatoka kando.
- Keki ya kakao inabaki huwa ni msingi wa chokoleti.
- Chokoleti nyeupe hutengenezwa kwa kutumia mafuta ya kakao pekee.
- Chokoleti ya kawaida huongezwa tena kiasi fulani cha mafuta yake.
- Chokoleti nyeusinyeusi hubaki bila nyongeza ya mafuta ya kakao.
- Chokoleti hukorogwa mara nyingi na maziwa na sukari kuwa pipi inayopendwa.