Caracalla
Kutoka Wikipedia
Caracalla (4 Aprili, 186 – 8 Aprili, 217) alikuwa Kaizari wa Dola la Roma kuanzia mwaka wa 209 hadi kifo chake. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Septimius Bassanius, na baadaye aliitwa Marcus Aurelius Severus Antoninus Augustus. Alimfuata baba yake, Septimius Severus ambaye alitawala pamoja naye hadi kifo cha baba tarehe 4 Februari, 211. Halafu Caracalla alitawala pamoja na kaka yake, Geta ambaye amemuua mwezi wa Desemba 211.