Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Bombomu - Wikipedia

Bombomu

Kutoka Wikipedia

Bunduki ya Gatling ilikuwa bombomu ya kwanza
Bunduki ya Gatling ilikuwa bombomu ya kwanza
Maxim ilikuwa modeli iliyopendwa kabla ya Vita Kuu I
Maxim ilikuwa modeli iliyopendwa kabla ya Vita Kuu I
Bombomu M2 na maganda matupu ya ramia
Bombomu M2 na maganda matupu ya ramia
Askari wawili Wamarekani na bombomu yao
Askari wawili Wamarekani na bombomu yao
Bombomu nzito kwenye manowari
Bombomu nzito kwenye manowari

Bombomu (au: bunduki ya mtombo; bunduki ya rashasha) ni silaha ya moto kubwa kiasi inayofyatulia risasi nyingi za mfululizo muda wote kiwashio cha silaha inashikwa hadi akiba ya ramia imekwisha.

Akiba ya ramia iko ama katika chemba yake au ramia zimepangwa katika ukanda unaopita kwenye bombomu. Bombomu ndogu hubebewa na askari mmoja lakini modeli nzito kiasi huhitaji watu wawili hadi watatu.

Bombomu ndogo zaidi huitwa bunduki ya nusu mtombo hutumiwa kama silaha ya kawaida ya askari lakini hutumia ramia za bastola. Ni nyepesi hailengi mbali sana na kusudi lake ni mapigano dhidi adui aliye karibu.

Bombomu kubwa zaidi hubebwa tena wa watu hufungwa juu ya gari au magurudumu huitwa mzinga wa bombom. Hutumiwa pia kwenye manowari na boti za kijeshi halafu kwenye ndege za kijeshi.

Yaliyomo

[hariri] Modeli za kwanza

[hariri] Mitrailleuse na Gatling

Mtangulizi wa bombomu ya kwanza ilikuwa "Mitrailleuse" iliyobuniwa Ubelgiji mnamo 1850. Ilikuwa na kasiba nyingi na kuzuungukwa kwa mkono. "Gatling" ya Marekani ilikuwa bombomu ya kwanza ilikuwa na kasiba sita na kuzungukuwa pia kwa kombo ya mkono. Wakati wa kuzunguka kasiba ya juu ilifyatulia risasi na mtambo ulijaza kasiba nyingine. Muundo huu uliachwa baadaye kwa sababu haikulenga vizuri. Lakini umerudi tena kwa bombomu zinazotumiwa katika ndege za kivita kwa sababu kasiba nyingi zinaruhusu kufyatulia risasi nyingi bila silaha kushika joto mno kwa sababu kila kasiba inapata nafasi ya kupoa tena.

[hariri] Maxim

Bombomu nyingi zilifuata muundo wa Maxim iliyopatikana tangu 1885 iliyotumia nishati ya marejeo nyuma baada ya kila pigo kuondoa ganda la ramia na kuweka ramia mpya katika silaha. Ilikuwa na kasiba moja tu. Ramia zilipangwa kwa ukanda uliopita katika silaha. Silaha ya Maxim ilikuwa ilikuwa bombomuy a kwanza iliyofaulu kijeshi ikawa chombo muhimu katika upanuzi wa kikoloni wa mataifa ya Ulaya huko Afrika na Asia pasipokuwa na teknolojia hiyo. Wakati wa vita ya Matebele nchini Zimbabwe 1893-1894 kikosi cha Waingereza 50 kilishinda askari 5,000 Wamatabele kwa kutumia bombomu za Maxim 4. Mshairi Mwingereza Hilaire Belloc alitunga shairi kuhusu vita za kikoloni akisema:

"Whatever happens, we have got
The Maxim gun, and they have not"

[hariri] Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia

Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia iliona jeshi kubwa zilizopigana zikitumia bombomu kila upande. Kuwepo kwa silaha hizi kulilazimisha mabadiliko katika mibino ya vita. Hadi wakati ule mashambulio yalitekelezwa kwa askari wengi walioshambulia maadui kwa mbio moja kwa moja. Mbinu huu ulisababisha vifo vingi kwa sababu bombomu zilipungua mno idadi ya washambuliaji kabala hawakufika mahali walipoelekea. Kwa hiyo vita hii iliona mbinu mpya askari wakiambiwa kuchimba mifereji na kusubiri hadi risasi za mizinga ziliponda kwa mifereji ya maadui kwa siku na wiki mfululizo hadi kujaribu shambulio upya.

Hata kubuniwa kwa vifaru ilikuwa tokeo moja ya hatari ya bombomu kwa sababu Waingereza walitafuta njia ya kushambulia mifereji ya Wajerumani kwa kumaliza bomubomu kwanza bila kupoteza askari wengi mno.

[hariri] Vita Kuu ya Pili ya Dunia

Vita hii iliona bombomu nyepesi zaidi zilizohitaji askari wawili mmoja wa kulenga na kupiga mwenzake wa kushughulika ramia. Iliona pia modeli za kwanza za bunduki ya nusu mtombo.

Vilevile modeli nzito zilipatikana kwa wingi katika ndege za kijeshi kwa kushambulia ndege za adui na pia watu ardhini.

Tatizo la silaha hizi ni joto linalojitokeza wakati wa kufyatulia risasi nyingi katika muda mdogo. Palikuwa na modeli zilizotumia mtambo wa maji ya kupuza kasiba lakini hii iliongeza uzito tena.

[hariri] Mitambo ya kisasa

Teknolojia imeendelea na kuunda bombomu nyepesi zinazobebwa na askari mmoja tu zikiwa na uwezo wa kufyatulia risasi nyingi kushinda zamani bila kukwama.

Katika matumizi ya kijeshi bunduki za askari wa kawaida zimepokea sifa za bombomu yaani uwezo wa kufyatulia mfululizo.

Modeli kubwa zinazohesabiwa kati ya mizinga iko kwa matumizi juu ya vifaru, kwenye manowari na ndege.

Teknolojia ya vita ya wakati ujao utaona mabadiliko zaidi. Mitambo kama miwani ya kuona usiku inaonyesha bombomu haraka kutokana na joto la kasiba. Hadi sasa ni nchi chache zinazotumia mitambo hii lakini kadiri inavyosambaa silaha inayong'aa kwenye mitambo hii itakuwa hasara.

Image:WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Bombomu" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Bombomu kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.

Wikimedia Commons ina media kuhusu:


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -