Berili
Kutoka Wikipedia
Berili ni elementi na metali ya udongo alkalini yenye namba atomia 4 na uzani atomia 9.01218 kwenye mfumo radidia. Alama yake ni Be. Jina latokana na neno la kigiriki βηρυλλος berillos linalotaja aina ya vito ambamo elementi hii iligunduliwa mara ya kwanza mwaka 1798 kama oksidi ya Berili.
Elementi tupu ina valensi mbili na rangi yake ni kijivu feleji. Ni metali ngumu sana na nyepesi. Katika kiwango sanifu cha joto na shindikizo berili haioksidishi kirahisi.
Kiasili inpatikana katika kampaundi mbalimbali. Aina zinazoonekana zaidi ni ndani ya mawe ya kito kama zumaridi.
Matumizi ya Berili ni hasa katika aloi za metali hasa pamoja na alumini na shaba.
Makala hiyo kuhusu "Berili" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Berili kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |