Alfabeti ya Kigiriki
Kutoka Wikipedia
Herufi za kawaida | ||||
---|---|---|---|---|
Α α Alfa | 1 | Ν ν Ni | 50 | |
Β β Beta | 2 | Ξ ξ Ksi | 60 | |
Γ γ Gamma | 3 | Ο ο Omikron | 70 | |
Δ δ Delta | 4 | Π π Pi | 80 | |
Ε ε Epsilon | 5 | Ρ ρ Rho | 100 | |
Ζ ζ Dzeta | 7 | Σ σ ς Sigma | 200 | |
Η η Eta | 8 | Τ τ Tau | 300 | |
Θ θ Theta | 9 | Υ υ Ipsilon | 400 | |
Ι ι Iota | 10 | Φ φ Phi | 500 | |
Κ κ Kappa | 20 | Χ χ Chi | 600 | |
Λλ Lambda | 30 | Ψ ψ Psi | 700 | |
Μ μ Mi | 40 | Ω ω Omega | 800 | |
Herufi za kihistoria | ||||
Digamma | 6 | San | 90 | |
Stigma | 6 | Sho | 90 | |
Heta | 8 | Qoppa | 90 | |
Yot | 10 | Sampi | 900 |
Alfabeti ya Kigiriki ni mwandiko wa kuandika lugha ya Kigiriki. Herufi zake hutumiwa pia kama alama za kisayansi. Ilianzishwa wakati wa ustaarabu wa Ugiriki ya Kale na imeendelea kutumiwa katika Ugiriki ya leo.
Alfabeti ya Kigiriki ni alfabeti mama ya lugha za Ulaya. Ni asili ya Alfabeti ya Kilatini ambayo ni mwandiko unaotumiwa zaidi duniani kushinda miandiko mingine. Ni pia asili ya alfabeti za Kikyrili na Kikopti. Kuna miandiko mingine ya kihistoria iliyotokana na Kigiriki.
Asili ya mwandiko huo ulikuwa alfabeti ya Kifinisia. Tofauti kubwa ni alama za vokali na baadaye badiliko la mwendo wa mwandiko kutoka kushoto kwenda kulia tofauti na Kifinisia iliyoandikwa kutoka kulia kwenda kushoto jinsi ilivyo hadi sasa katika mwandiko wa Kiarabu na Kiebrania ambazo ni lugha za kisemiti jinsi ilivyokuwa Kifinisia.
Sehemu ya herufi zilizopokelewa kutoka Kifinisia ziliachwa baadaye kwa sababu lugha haikuwa na sauti za kulingana. Tangu mwaka 300 KK sehemu ya juu ya alfabeti inayoonyeshwa kwenye sanduku ilikuwa herufi za kawaida na alama za chini hazikutumiwa isipokuwa alama za namba.
Katika historia ndefu ya alfabeti hii matamshi ya alama yamebadilika pamoja na mabadiliko ya lugha yenyewe. Mwanafunzi wa Kigiriki cha Kale anayesoma maandiko ya Plato au vitabu vya Agano Jipya katika lugha asilia ataona matataizo akija Ugiriki na kuwasikia Wagiriki wa leo hata kama anaweza kusoma maandishi yote hataelewa mengi.
[hariri] Maana ya namba
Kila herufi ilikuwa pia na matumizi kama namba kwa sababu Wagiriki wa Kale hawakuwa na alama za pekee za namba. Herufi tatu za kihistoria ambazo hazikutumiwa tena kwa maandishi ziliendlea kama alama za namba yaani Digamma au Stigma = 6 (alama ς), Koppa = 90 (alama ϙ au ϟ) na Sampi = 900 (alama ϡ au kama kwenye sanduku).
Kwa kutofautisha herufi na namba alama yake ilipewa mstari mdogo juu yake kama αʹ = 1, βʹ = 2, γʹ = 3. Kwa namba kuanzia 1,000 mstari upande wa kushoto uliongezwa, kwa mfano ͵α = 1,000, ͵β = 2000, ͵βηʹ = 2008.
[hariri] Matumizi ya Kisayansi
Herufi za Kigriki zatumiwa sana katika hesabu na sayansi. Mifano inayojulikana zaidi ni matumizi ya α, β na γ kama majina ya pembe za pembetatu.
Katika mahesabu ya duara namba π (pi) ni muhimu sana.
Kuna matumizi mengi mengine karibu kila herufi ina maana fulani kisayansi.