Pembetatu
Kutoka Wikipedia
Pembetatu ni umbo bapa lenye pande tatu zisizonyoka na kukutana kwenye pembe tatu za kila kona.
Jumla ya kiwango cha pembe zote tatu ni nyuzi 180. Eneo la pembetatu ni nusu kitako mara kimo.
Pembe zatajwa kwa kawaida kwa herufi za kwanza katika alfabeti ya Kigiriki yaani alfa, beta na gamma.
[hariri] Aina za pembetatu
Pembetatu hupangwa kufuatana na tabia za pande zao:
- Kwenye pembetatu pandesawa pande zote tatu ni sawa.
- Kwenye pembetatu pacha pande mbili ni sawa.
- Kwenye pembetatu mshatu pande zote ni tofauti.
pandesawa | pacha | mshatu |
Pembetatu hupangwa pia kufuatana na tabia za pembe zao:
- Pembetatu mraba ina pembe moja ya 90°.
- Pembetatu butu ina pembe moja ambayo ni kubwa ya 90°.
- Pembetatu kali ina pembe ambazo zote ni ndogo kuliko 90°.
- Pembetatu mshazari ni kila pembetatu isiyo mraba.
mraba | butu | kali |
mshazari |