Albert Claude
Kutoka Wikipedia
Albert Claude (24 Agosti, 1898 – 22 Mei, 1983) alikuwa daktari kutoka nchi ya Ubelgiji, na pia alikuwa na uraia wa Marekani tangu 1941. Hasa alichunguza vipengele mbalimbali vya chembe hai. Mwaka wa 1974, pamoja na George Palade na Christian de Duve alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.